Dodoma FM

Vijana waomba huduma rafiki elimu ya afya ya uzazi

28 April 2026, 14:03

Vijana wanatamani kupata huduma rafiki za afya ya uzazi ambazo zitawafanya kuwa huru.Picha na Michuzi.

Hali ya mazoea na fikra za kuamini kuwa clinik ni sehemu ya watoto na akina mama kunapelekea wao kuwa na aibu ya kufika na kukaa eneo hilo kusubiri huduma.

Na Victor Chigwada.

Imeelezwa kuwa licha ya elimu na kampeni mbalimbali zinazo tolewa na wizara ya afya kuhusu afya ya uzazi bado muitikio wa vijana hususani vijijini kujitokeza kupata elimu hiyo na kuwapeleka wenza wao kliniki ni mdogo sana.

Taswira ya habari iliwatafuta baadhi ya vijana na kuzungumza nao ambapo wanasema kuwa  wanashindwa kwenda kwenye vituo vya afya kupata elimu ya afya ya uzazi na kuwasindikiza wenza wao kutokana na eneo la cliniki kuzoeleka kuwa ni eneo la mama na mtoto.

baadhi ya vijana wanadai kuwa hali ya mazoea na fikra za kuamini kuwa clinik ni sehemu ya watoto na akina mama kunapelekea wao kuwa na aibu ya kufika na kukaa eneo hilo kusubiri huduma.

Sauti za vijana.

Aidha wameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi  wanasema kitendo cha serikali kuajiri vijana katika huduma za uzazi na katika huduma za afya ngazi ya jamii kunaweza kuwavuta wao kuhudhuria clinic bila hofu yoyote na kuwa wawazi kwa wahudumu hao.

Vijana hao wameiomba serikali kutambua kuwa kundi la vijana linahitaji elimu zaidi hasa elimu ya afya ya uzazi hivyo ni muhimu kuweka mazingira rafiki kwa vijana kupata huduma hizo bila kikwazo chochote.

Sauti za vijana.