Dodoma FM

Sekta ya bima kuchangia asilimia 3 ya pato la Taifa

30 June 2026, 16:47

Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Bancassurance wa Alliance, Tumaini Pyanisa,akiongea katika uzinduzi wa ofisi ya mauzo ya Kampuni ya Bima ya Alliance jijini Dodoma.Picha na Bennard Filbert.

TIRA inaendelea kusimamia sekta ya bima kwa kulinda maslahi ya wateja na kuimarisha huduma, ikiwa ni sehemu ya kufikia lengo la serikali la asilimia 3 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2030.

Na Bennard Filbert.

Kufikia mwaka 2030, Serikali inalenga sekta ya bima kuchangia asilimia 3 ya Pato la Taifa kupitia ongezeko la matumizi ya huduma za bima nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Mipango na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Edgar Shao, kwaniaba ya Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware, baada ya uzinduzi wa ofisi ya mauzo ya Kampuni ya Bima ya Alliance jijini Dodoma.

Amesema kwa sasa sekta ya bima inachangia asilimia 2.18 ya Pato la Taifa, hali inayo onyesha Taifa liko kwenye njia nzuri ya kufikia lengo la mwaka 2030.

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kutumia huduma za bima ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi.

Sauti ya Edgar Shao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Bancassurance wa Alliance, Tumaini Pyanisa, amesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo Dodoma kutasogeza huduma za bima karibu na wananchi.

Sauti ya Tumaini Pyanisa