Dodoma FM

Je masomo ya ziada yana mchango gani wakati wa likizo

12 June 2026, 12:33

Je masomo ya ziada yanawajenga watoto wakati wa likizo.Picha na Mtandao.

Wanasema msisitizo mkubwa wa masomo bila mapumziko unaweza kuleta uchovu wa kiakili kwa wanafunzi, hivyo ni muhimu kupanga vipindi visivyowalemaza watoto.

Na Daniel Njau.

Wakati wanafunzi wakiwa kwenye likizo za shule, baadhi ya wazazi na wataalamu wa elimu wanaona kuwa masomo ya ziada yana mchango mkubwa katika kuwasaidia watoto kuendeleza maarifa yao, kurekebisha maeneo yenye changamoto kitaaluma na kujiandaa vyema kwa muhula unaofuata wa masomo.

Baadhi ya wazazi na walezi wamesema kuwa masomo ya ziada kipindi cha likizo huwasaidia watoto kutopoteza mwelekeo wa masomo waliyojifunza shuleni.

Wameeleza kuwa bila kuwa na muda maalumu wa kujifunza, wanafunzi wengi hujikuta wakisahau baadhi ya mambo muhimu waliyojifunza darasani.

Sauti ya kina Daniel.

Kwa upande mwingine, baadhi ya wazazi wamebainisha kuwa masomo ya ziada wakati wa likizo yanapaswa kuwa na uwiano ili watoto pia wapate muda wa kupumzika na kushiriki shughuli za kijamii na michezo.