Dodoma FM

Rais Samia kuzindua benki ya ushirika Dodoma

25 April 2025, 5:36 pm

Picha na mkuu wa mkoa na viongozi wengine wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa benki hiyo.Picha na Alfred Bulahya.

Hata hivyo ametoa wito Kwa wananchi wote wa Dodoma na maeneo jirani kujitokeza Kwa wingi na uzalendo kushiriki katika tukio hilo la kihistoria.

Na Alfred Bulahya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Benki ya Ushirika Tanzania(COOP Bank Tanzania) Aprili 28 mwaka huu jijini Dodoma.

Pia Rais Samia atatembelea makao makuu ya Benki hiyo na kukagua maonesho ya Ushirika yatakayofanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 25,2025 Jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,amesema kabla ya uzinduzi wa Benki, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa atazindua Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Aprili 27 mwaka huu.

Sauti ya mh.Rosemery Senyamule.

Aidha amesema kuwa washiriki wa mkutano huo ni viongozi wa kitaifa,wadau wa ushirika kutoka ndani na nje ya nchi,Wafanyabiasha na wananchi wa kawaida.