

12 December 2024, 5:12 pm
Kila ifikapo tarehe 10 Desemba ni Siku ya Haki za Binadamu na pia ni kilele cha siku 16 za harakati za kupinga ukatili wa kijinsia .
Na Annuary Shaban.
Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania na wadau wengine wamewasisitiza wanaume kujitokeza kutoa taarifa za ukatili pindi wanapofanyiwa.
Akizungumza katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili Neema Ahmed, Wakili na Mratibu Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania, ametaja sehemu sahihi ambazo wanaume wanaweza kutoa taarifa za ukatili kwa uhuru.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi. Salome Chilongani amesema kuwa familia nyingi zimekuwa zikitelekezwa na wanaume kutokana na utelekezaji wa sababu mbalimbali.
Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamesema kuwa jukwaa hilo limekuwa nyenzo muhimu katika kuelimisha kuhusu masuala mazima ya ukatili wa kijinsia.