Dodoma FM

Wananchi Nholi waiomba serikali kukamilisha ujenzi wa Zahanati

17 April 2026, 5:08 pm

Wananchi hao wanalazimika kutembea umbali mrefu na wagonjwa ili kuwafikisha Mpalanga kupata huduma za matibabu.Picha na Mtandao.

Changamoto ya kukosa zahanati imekuwa ikipelekea wakazi wa Nholi kutembea umbali mrefu kufika makao makuu ya Kata Kijiji Cha Mpalanga.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Nholi Kata ya Mpalanga Wilayani Bahi wameiomba Serikali kukamilisha zahanati inayojengwa kijijini hapo .

Changamoto ya kukosa zahanati imekuwa ikipelekea wakazi wa Nholi kutembea umbali mrefu kufika makao makuu ya Kata Kijiji Cha Mpalanga ambalo ndipo huduma za afya zinapo patikana.

Wakiongea na Taswira ya habari wakazi hao wamesema  wanalazimika kutembea umbali mrefu na wagonjwa ili kuwafikisha Mpalanga kupata huduma ya matibabu hali inayo hatarisha usalama wa wagonjwa hao hasa akina mama wajawazito.

Sauti za wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nholi Bi.Caroline Mtuli amesema kwasasa wanafanya utaratibu wa kumalizia ujenzi wa Zahanati hiyo ili kuwasogezea wananchi huduma za afya karibu.

Sauti ya Bi.Caroline Mtuli.