Waziri Kapinga aipongeza Mainland kwa uwekezaji mkubwa
26 June 2026, 12:48

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo maboresho ya sera, sheria na mifumo ya kodi ili kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vya mafuta ya kula na kuongeza uzalishaji wa ndani.
Na Mariam Kasawa.
Serikali imeahidi kuendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda ili kuchochea ukuaji wa uchumi hapa Nchini.
Hayo yamesemwa na waziri wa viwanda na biashara mh.Judith Kapinga alipotembelea katika kiwanda cha kuchakata na kuzalisha mafuta ya kula Mainland kilichopo Veyula jijini Dodoma ambapo katika ziara hiyo waziri Kapinga amejionea shughuli mbalimbali zinazo fanyika kiwandani hapo.
Waziri Kapinga amesema viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya ndani vina nafasi muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa pamoja na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Amesema Serikali imeanza kushirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na taasisi zake kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta ili kuhakikisha viwanda vinapata malighafi za kutosha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Jiaweli Chen, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kutoa ushirikiano unaowezesha viwanda kufanya kazi kwa ufanisi amesema hatua hiyo inaonesha utayari wa viongozi kushirikiana na sekta binafsi katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli za uzalishaji.
Akiongea mara baada ya kutamatika kwa ziara hiyo mkurugezi wa Mawasiliano katika kiwanda hicho cha Mainland Bi. Betty Mkwasa amemesema kiwanda hiki kimetoa fursa kubwa kwa vijana kupata ajira ambapo hadi sasa zaidi ya vijana 400 wameajiriwa katika kiwanda hicho .
Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo maboresho ya sera, sheria na mifumo ya kodi ili kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vya mafuta ya kula na kuongeza uzalishaji wa ndani.