Dodoma FM

Wanufaika TASAF wapatiwa bima za Afya

3 June 2026, 16:48

Sasa watanufaika kupitia bima za afya ambapo wataondokana na adha ya kulipa gharama za matibabu mara kwa mara.Picha na Mtandao.

familia zenye kipato kidogo kushindwa kumudu gharama za matibabu wanapo umwa hivyo kupitia msaada huo wa bima za afya utawasaidia kupata matibabu kwa wakati.

Na Victor Chigwada.

Wanufaika wa mfuko wa kusaidia kaya maskini TASAF kijijini Chilonwa wailayani Chamwino wameishukuru serikali kwa kuanza utaratibu wa kuwapatia bima za afya kwaajili ya matibabu.

Wamesema kuwa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kunapelekea baadhi ya familia zenye kipato kidogo kushindwa kumudu gharama za matibabu wanapo umwa hivyo kupitia msaada huo wa bima za afya utawasaidia kupata matibabu kwa wakati.

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Chilonwa Bw.Esau Lekadi amesema mfuko wa kusaidia kaya maskini TASAF katika kijiji hicho umesaidia kubadilisha maisha ya wanufaika na sasa watanufaika kupitia bima za afya ambapo wataondokana na adha ya kulipa gharama za matibabu mara kwa mara.

Bw.Esau Lekadi