Dodoma FM
Green Samia kutoa elimu ya mazingira kwa vijana
9 September 2024, 7:51 pm
Na Mariam Kasawa. Bwn. Reuben Chacha mhandisi wa mazingira kutoka mkoani Iringa anasema kijana ni muathirika namba moja katika mabadiliko ya tabianchi kutokana na shughuli wanazo fanya ambazo si rafiki kwa mazingira hivyo kupelekea mabadiliko ya tabianchi.
Amesema kupitia vijana wamekuja na kampeni ya Green Samia itakayo wezesha vijana katika mikoa yote nchini kufundishwa mbinu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na utunzaji wa mazingira.
Nao baadhi ya vijana wadau wa mazingira wanasema vijana ni kundi kubwa lenye nguvu na ushawishi hivyo kupitia vijana ajenda ya mabadiliko ya tabianchi itafika kwa kila mtu na kila mtu atatambua umuhimu wa kutunza mazingira.
Madau wa mazingira