Dodoma FM

Wanaume Dodoma waonywa kuacha ukatili wa kiuchumi kwa wake zao

18 March 2024, 12:05 pm

Picha ni wa vyama vya ushirika jijini Dodoma akiongea na wananchi wa kata ya Mpunguzi.Picha na Fred Cheti.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa hamasa kwa wananchi hususani wanawake kujiunga na vyama vya ushirika.

Na Fred Cheti.

Wanaume wametakiwa kuacha kufanya ukatili wa kiuchumi kwa wake zao hasa kwenye kilimo ambapo inaelezwa kuwa baadhi ya wanaume wamekua hawawashirikishi wake zao katika uuzaji wa mazao licha ya kulima kwa pamoja.

Hayo yameelezwa na Mrajisi wa vyama vya ushirika jijini Dodoma wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mpunguzi kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wananchi hao hasa wanawake kujiunga na vyama vya ushirika.

Sauti ya Mrajisi wa vyama vya ushirika jijini Dodoma.
Picha ni wakazi wa Mpunguzi wakiwa katika mkutano huo . Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wao nao baadhi ya wananchi katika kata hiyo ya Mpunguzi wamesema suala hilo limekua likirudisha Maendeleo mwanamke nyuma kutokana na kutumia nguvu lakini wanashindwa kuendelea kutokana na jambo hilo.

Sauti za wananchi.