Dodoma FM

Ekari 20 za mazao zafyekwa na wafugaji Kiteto

21 May 2025, 4:31 pm

Picha ni wakazi wa kijiji cha Chekanao wilayani Kiteto mkoani Manyara wakizungumzia uharibifu huo wa mazao. Picha na Kitana Hamis.

Wakazi wa kijiji hicho wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ili wafugaji hao wapate sehemu za malisho.

Na Kitana Hamis.
Zaidi ya Ekari 20 za shamba lenye mazao ya mahindi na alizeti za kulima Twalib Shaban zimefyekwa na wafugaji wa jamii ya kimasai kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Chekanao Wilayani Kiteto Mkoani Manyara ambapo wananchi wa kijiji hicho wanadai kuwa kundi hilo la wafugaji jamii ya wamasai wamekuwa wakifanya vitendo hivyo hali inayo weza kuleta njaa kijijini hapo.

Wananchi hao wameomba serikali itafute njia mbadala ili wafugaji hao wapate sehemu za malisho kwani kutokana na kkukosa malisho ya mifugo yao wanajikuwa wanavamia mashamba ya wakazi wa eneo hilo na kulisha mifugo.