Dodoma FM
Dodoma FM
5 May 2026, 16:40

Hii inafanya uwekezaji katika huduma na programu za afya ya vijana kuwa si tu jambo la kimaadili bali pia ni jambo lenye maana kiuchumi.
Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) uwekezaji wa haraka unahitajika ili kukabiliana na changamoto za kiafya zinazoongezeka kwa vijana barubaru ikiwemo kuhakikisha mahitaji ya afya ya akili pamoja na afya ya uzazi kwa vijana bilioni 1.3 duniani kote yanatimizwa.
Kulingana na ripoti hiyo, ujana ni hatua ya kipekee na muhimu katika maendeleo ya binadamu, ambapo misingi ya afya bora ya muda mrefu huwekwa.
Ripoti hiyo Mpya ambayo imezinduliwa hivi karibuni imebainisha uwepo wa wasiwasi kwenye afya ya vijana kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, ikionesha hitaji la hatua za haraka.
Takribani kijana mmoja kati ya vijana 7 duniani wanakabiliwa na matatizo ya afya ya akili kama vile unyogovu(depression) na wasiwasi(anxiety). Aidha, kiwango cha upungufu wa damu kwa wasichana vijana hakijabadilika tangu mwaka 2010, huku karibu kijana mmoja kati ya vijana 10 wakiwa wanakabiliwa na Unene kupita kiasi.