Utupaji taka holela wakithiri Miyuji
12 August 2026, 17:56

Kwa mujibu wa UN-HABITAT wanasema kwamba taka zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya umma, mazingira na hali ya hewa, lakini katika zama hizi sayansi, teknolojia na ubunifu wa hali ya juu vinaweza kuleta suluhu ya gharama nafuu katika changamoto hiyo ya taka na kuisaidia miji na jamii kuziona taka kama ni fursa ya biashara.
Na Godson Mgima.
Utupaji holela wa taka umeendelea kuwa changamoto katika eneo la mipango katika kata ya miyuji, hali inayowafanya baadhi ya wakazi kutupa taka katika maeneo ya wazi.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanasema tatizo hilo limekuwa likiwapa usumbufu katika maisha yao ya kila siku, huku wakitaja harufu, uchafu na kuongezeka kwa taka katika maeneo wanayoishi.
Wamesema tatizo hilo linahitaji ushirikiano kati ya wananchi wenyewe na viongozi wa eneo ili kuhakikisha taka hazigeuki kuwa sehemu ya kawaida ya mazingira yao.
Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Miyuji Bw. Haward Mbogela, amesema: “Tatizo la taka linahitaji kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake huku akiwaasa wananchi kuacha taka ovyo.