Dodoma FM

Wenye ulemavu wa Polio watoa wito wa chanjo kwa watoto

24 August 2026, 18:02

Wamesema chanjo hiyo ni njia muhimu ya kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa polio.Picha na Stephen Noel.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa wazazi, walezi na jamii ni muhimu katika kuhakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanafikiwa.

Na Stephen Noel.

Watu wenye ulemavu wa kudumu uliosababishwa na ugonjwa wa polio wilayani Mpwapwa wamewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya polio ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo.

Wamesema polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vinavyoathiri mfumo wa fahamu na unaweza kusababisha baadhi ya wagonjwa kupooza na kupata ulemavu wa kudumu.

Kandido Mnemele na Miraji Athumani, wakazi wa Mpwapwa wenye ulemavu wa kudumu uliosababishwa na polio, wametoa wito huo wakati wa mahojiano maluumu na Dodoma Fm  ikiwa zoezi Hilo linaenda kutekelezwa wilayani hapa.

Wamesema chanjo hiyo ni njia muhimu ya kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa polio na kumuepusha na madhara yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Thomas Rutachunzibwa, amesema wilayani Mpwapwa wanatarajia kuwafikia watoto 135,000 katika zoezi hilo la chanjo.

Amesema mkoa umejiandaa kwa vifaa na mahitaji muhimu kwa ajili ya kuhakikisha zoezi la utoaji wa chanjo linafanyika kwa ufanisi.

Sauti ya Noel.