Dodoma FM

Wanaume wanamchango na nafasi gani katika suala la uzazi wa mpango?

25 September 2026, 16:02

Picha ni Wanandoa wakipokea ushauri wa daktari kuhusu umuhimu wa kupanga uzazi salama kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango. Picha na Mwananchi.

Ushiriki wa wanaume katika masuala ya uzazi wa mpango ni muhimu katika kuhakikisha wanandoa na familia zinafanya maamuzi sahihi kuhusu idadi na muda wa kupata watoto.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Bi Itika Shemwela, yeye ni Mratibu wa Afya ya Uzazi wa Mpango Dodoma Jiji, amesema wanaume wana nafasi kubwa katika kutoa ushirikiano na kushiriki katika maamuzi yanayohusu uzazi wa mpango, badala ya kuliacha suala hilo kuwa jukumu la wanawake pekee.

amesema bado baadhi ya jamii zinakabiliwa na mfumo dume unaoweza kuwafanya wanaume kuwa na ushawishi mkubwa katika maamuzi ya uzazi wa mpango, huku wanawake wakati mwingine wakikosa nafasi ya kutoa maoni yao.

Hali hiyo inaonesha umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wanaume washiriki kwa uelewa na ushirikiano katika masuala ya uzazi wa mpango kwa manufaa ya familia.