Dodoma FM

Wenye vitiligo wahimizwa kujikinga na mionzi ya jua

13 August 2026, 17:50

Wataalamu wa afya wanasema maeneo yaliyoathirika na vitiligo huwa na upungufu wa melanin. Picha na mtandao.

Wataalamu wanasisitiza umuhimu wa watu wanaoishi na vitiligo kuendelea kufuatilia afya ya ngozi zao na kupata ushauri wa kitaalamu pale wanapohitaji.

Na Husna Munisi.

Watu wanaoishi na ugonjwa wa vitiligo wametakiwa kuzingatia utunzaji wa ngozi zao, hususan kujikinga dhidi ya mionzi ya jua, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na upungufu wa kinga ya asili ya ngozi katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.

Wataalamu wa afya wamesema maeneo yaliyoathirika na vitiligo huwa na upungufu wa melanin, rangi inayosaidia kulinda ngozi dhidi ya madhara yanayosababishwa na mionzi ya jua.

Dkt. Rahel Kilimba anashauri mambo ambayo mtu anayeishi na vitiligo anapaswa kuzingatia katika kutunza ngozi yake, ikiwemo namna sahihi ya kujikinga dhidi ya mionzi ya jua.

Aidha, watu wanaoishi na vitiligo wanashauriwa kuepuka kuchubua au kujeruhi ngozi bila sababu, pamoja na kufika katika kituo cha afya kwa ushauri wa kitaalamu iwapo wataona mabadiliko mapya au matatizo yoyote kwenye ngozi.

Kwa upande wake, Clementine Chalamila, mmoja wa watu wanaoishi na vitiligo, anaeleza namna anavyojitunza na kuitunza ngozi yake, akisisitiza umuhimu wa kuwa makini na bidhaa zinazotumika kwenye ngozi.

Sauti na Husna Munisi.