Wananchi watakiwa kuwa makini na fursa za mitandaoni
10 August 2026, 15:55

Wananchi wametakiwa kutokubali tamaa za fursa zinazoonekana kuvutia mitandao bila kuzichunguza huku wakihimizwa kutoa taarifa mapema wanapobaini viashiria vya utapeli au usafirishaji haramu wa binadamu.
Na Anwary Shaban.
Katika kipindi ambacho mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku wananchi wametakiwa kuwa makini na taarifa na fursa wanazokutana nazo mitandaoni hususani zinazohusisha ajira,safari na ahadi za maisha bora, ili kuepuka kuangukia mtego wa usafirishaji haramu wa binadamu.
Wito huo umetolewa na Afisa ustawi wa jamii kutoka sekretarieti ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu wizara ya mambo ya ndani ya nchi Bw.Miata Agustino ambapo amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakidanganywa kupitia mitandao ya kijamii na kupewa ahadi za uwongo.
Aidha amesema pamoja na usafirishaji haramu wa binadamu, mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika pia na baadhi ya matapeli kutengeneza akaunti bandia zinazofanana na za tasisi mbalimbali huku wengine wakitangaza nafasi za ajira zisizo halali kwa lengo la kuwatapeli.
kwa upande wao baadhi ya wananchi na wakazi wa Dodoma wameeleza kuwa wamewahi kukutana na tangazo la ajira safari na fursa nyingi za mitandaoni na wamekua wakichunguza baadhi ya taarifa izo na kuweza kuepukana nazo .