Dodoma FM

LATRA yafafanua usafirishaji wa mizigo ya Abiria

20 February 2023, 2:08 pm

Afisa mfawidhi LATRA Bw. Ezekiel Emmanuel akielezea utaratibu wa usafirishaji wa mizigo. Picha na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.

Akizungumza na Taswira ya habari Ezekiel Emmanuel Afisa Mfawidhi  Latra amesema abiria anaposafiri na mzingo ni wajibu wa  msafirishaji kusafirisha bure endapo unakidhi viwango.

Kwa mujibu wa kanuni ya 37 ni wajibu wa msafirishaji wa gari la abiria kumsafirishia abiria mzigo wake bure kama hauzidi kilo 20.

Katika hatua nyingine amezungumzia watu wenye ulemavu juu ya vifaa vyao vinavyowawezesha kutembea mara baada ya kushuka katika vyombo vya usafiri.

Sauti ya Ezekiel Emmanuel.