Dodoma FM

Huduma ya maji nchini sasa 88% mijini, 77% vijijini

9 June 2023, 12:44 pm

mkurugenzi msaidizi idara ya usambazaji maji na usafi wa mazingira kutoka wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri. Picha na Dodoma Tv.

Aidha ametoa wito kwa jamii kuzingitia sheria na kulinda miundombinu ya maji ili kuunga mkono jitihada za upatikanaji wa huduma ya maji nchini.

Na Alfred Bulahya.

Imeelezwa kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji nchini imeendelea kuimarika na kufikia asilimia 88 kwenye maeneo ya mijini mwaka 2023, kutoka 84 mwaka 2020 huku vijijini ikifikia asilimia 77 mwaka 2023 kutoka asilimia 70.1 mwaka 2020.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi msaidizi idara ya usambazaji maji na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, wakati akizungumza katika kipindi cha the Morning Power show kinachorushwa na Dodoma Tv.

Mhandisi Mwajuma amesema kuimarika kwa huduma ya maji kunatokana na utekelezaji wa mipango mikakati mbalimbali ambapo hadi sasa tayari serikali imetekeleza miradi 1373 kwenye maeneo ya vijini huku mingine 80 ikitekelezwa katika maeneo ya mjini.

Sauti ya mkurugenzi msaidizi idara ya usambazaji maji .

Ameitaja baadhi ya miradi inayotarajia kutekelezwa kuwa ni pamoja na mradi wa Bwawa la Farkwa na Lake Tanganyika itakayotoa huduma ya maji katika mkoa wa Dodoma.

Sauti ya mkurugenzi msaidizi idara ya usambazaji maji .