Dodoma FM

Ujenzi wa bweni la wasichana Mpendoo lita wanusuru na vitendo hatarishi

26 July 2023, 5:26 pm

Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mpendoo likiwa limekamilika. Picha na Fred Cheti.

Ujenzi wa bweni hilo unatarajia kupunguza adha kwa wanafunzi hao katika shule hiyo kutokana  wengi kutembea  umbali mrefu hadi shuleni hapo hali inayohatarisha usalama wao.

Na Fred Cheti.

Kukamilika wa kwa ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Mpendoo wilayani Chemba  kunatarajia kupunguza adha kwa wanafunzi hao katika shule hiyo kutokana  wengi kutembea  umbali mrefu hadi shuleni hapo hali inayohatarisha usalama wao.

Hayo yameelezwa na Mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana Gilialu Gisiri wakati akifanya mahojiano  na Dodoma TV ambae ni mmoja wa wasimamizi wa utekelezaji wa  ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa madarasa na mabweni hayo kupitia mradi (BOOST) unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mpendoo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana Gilialu Gisiri akizungumza na Dodoma Tv kuhusu ujenzi wa bweni hilo. Picha na Fred Cheti.

Aidha Mwalimu huyo ametoa wito  kwa wazazi kuwapatia ushirikiano wanafunzi hao wa kike ikiwemo kuwapa mahitaji yote ya  msingi pindi wanapoingia katika bweni hilo huku akitoa wito kwa serikali kuwasaidi kujenga bweni la wanafunzi wa kiume pia.

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mpendoo.