Dodoma FM

Ratiba ya kumuaga Hayati, Rais Dkt. John Pombe Magufuli

20 March 2021, 8:48 am

Na, Mariam Kasawa.

Ratiba ya kumuaga hayati Mh, Dkt John Pombe Magufuli yabadilika , Zanzibar nayo itapata nafasi ya kumuaga Kwa mujibu wa mabadiliko ya ratiba Hayati Dkt John Magufuli atazikwa tarehe 26 na si 25 iliyo kuwa imetangazwa hapo awali .

Kwa mujibu wa ratiba itakuwa kama ifuatavyo,

Machi 20 Dar es salaam , viongozi kutoa heshima za mwisho,

Machi 21 Dar es salaam , Wananchi kutoa heshima za mwisho.

Machi 22 Dodoma, wananchi kutoa heshima za mwisho.

Machi 23 Zanzibar, Wananchi kutoa heshima za mwisho.

Machi 24 Mwanza, Wananchi kutoa heshima za mwisho.

Machi 25 Chato, Wananchi na familia kutoa heshima za mwisho.

Machi 26 Chato, Mazishi.