Dodoma FM

Kuondolewa kwa sheria ya kushusha mizigo Job Ndugai kwaleta neema kwa wafanyabiashara

14 November 2023, 3:29 pm

Picha ni Mwenyekiti wa soko kuu Majengo Bw. Godfrey Rwegazama akiongea na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara katika soko kuu la majengo jijini Dodoma pamoja na soko la sabasaba walikuwa wakishusha mizigo yao katika soko la Job Ndugai na katika siku za hivi karibuni Jiji la dodoma liliruhusu wafanyabiashara kushusha mizigo katika masoko yao.

Na Khadija Ibrahim.

Kufuatia uongozi wa Jiji la Dodoma kuruhusu wafanyabiashara kushushia mizigo katika eneo la soko baadhi ya wafanyabiashara na wabeba mizigo katika soko la majengo wameiomba serikali kuongeza muda wa kushusha mizigo.

Awali wafanyabiashara walikuwa wakishushia mizigo yao katika eneo la soko kuu la Job Ndugai ambapo ilikuwa ni chanagamaoto katika suala la usafirishaji na gaharama kuwa kubwa.

Picha ni mmoja wa wabeba mizigo sokoni hapo akiongea na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Dodoma tv imewatembelea baadhi ya wafanyabiashara katika soko kuu la majengo jijini Dodoma kufahamau ni kwa namna gani wamenufaika na hatua hiyo ingawa kwa upande wa wabeba mizigo hali ni tofauti.

Sauti za baadhi ya wafanyabiashara na wabeba mizigo.

Aidha dodoma tv imefanya mahojinao na mwenyekiti wa soko kuu la majengo jijini dodoma juu ya suala hilo ambapo hapa akawa na haya ya kusema.

Sauti ya mwenyekiti wa soko kuu la majengo.