Dodoma FM

Ukosefu wa Dawa katika Zahanati ya kijiji cha Champumba

24 February 2023, 4:20 pm

Ukosefu wa Dawa katika Zahanati ya kijiji cha Champumba wilayani Chamwino.Picha na Mtanzania

Licha ya kupata huduma katika zahanati ya kijiji cha Champumba wilayani Chamwino lakini bado kasi ya upatikanaji dawa imekuwa ni ndogo.

Na Victor Chigwada.

Ukosefu wa Dawa katika Zahanati ya kijiji cha Champumba wilayani Chamwino imetajwa kuwa sababu ya wananchi kushindwa kujiunga na bima za afya
Pia inaelezwa kuwa Morali ya wananchi imezidi kushuka Licha ya uwepo wa zahanati hiyo katika kijiji hicho
Taswira ya Habari imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.John Mdabaji amesema kuwa licha ya kupata huduma katika zahanati hiyo lakini bado kasi ya upatikanaji dawa imekuwa ni ndogo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji Bw.John Mdabaji.

Vilevile ametaja changamoto nyingine katika zahanati hiyo ni idadi ndogo ya watumishi iliyopo hali inayosababisha kuongeza kwa changamoto pindi wanapotoa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji Bw.John Mdabaji.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Bw.Wiliamu Teu akizungumzia changamoto hiyo ndani ya zahanati hiyo amesema hali ya ukosefu wa dawa ipo na imesababisha kupunguza kasi ya wananchi kujiunga na bima za afya na wakati mwingine wenye bima kushindwa kupata huduma stahiki
Teu ameiomba Serikali kuwaongezea watumishi wa afya pamoja na kuhakikisha hali ya upatikanaji wa dawa una imarika katika zahanati hiyo.

Sauti ya Diwani Bw.Wiliamu Teu