Dodoma FM

NEMC na Halmashauri ya jiji la Dodoma zaagizwa kufanya tathhmini katika milima

15 March 2024, 6:16 pm

Picha ni eneo la Iyumbu Kata ya Iyumbu Jijini Dodoma ambalo mazingira yake yameharibiwa kutokana na uchimbaji wa madini na ujenzi.Picha na Mariam Kasawa.

kwa mujibu wa sheria ya mazingira ibara ya 58 ibara ndogo ya 2 kifungu kidogo cha D Kinatoa maelekezo ya kulinda vilima vyote vya jiji la Dodoma.

Na Mariam Kasawa.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimeagizwa kufanya tathimini ya hali ya kimazingira katika milima yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa kipindi cha wiki mbili.

Kauli ya metolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Seleman Jafo baada ya kutembelea eneo la Iyumbu Kata ya Iyumbu Jijini Dodoma na kutoridhishwa na hali ya uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchimbaji wa madini na ujenzi katika eneo hilo.

Sauti ya Mh. Jafo.
Picha ni eneo la Iyumbu Kata ya Iyumbu Jijini Dodoma ambalo mazingira yake yameharibiwa kutokana na uchimbaji wa madini na ujenzi.Picha na Mariam Kasawa.

Afisa maliasili na mazingira jiji la Dodoma Vedastus Milinga anasema wameshachukua hatua ikiwemo kufuta vibali vya uchimbaji.

Sauti ya Vedastus Milinga.