Dodoma FM

Jeshi la polisi laanza uchunguzi madai ya raia kunyanyaswa na maaskari

21 December 2023, 4:52 pm

Picha ni Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msadizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime. Picha na Jeshi la Polisi.

SACP Misime amewaomba wananchi wenye ushahidi kulingana na malalamiko yalivyowasilishwa na walalamikaji katika mitandao ya kijamii asisite kujitokeza ili uchunguzi huo ukamilike mapema na hatua zingine za kisheria zifuate.

Na Mariam Kasawa.
Jeshi la polisi limesema kuwa limeanza kufanyia uchunguzi malalamiko yaliyotolewa na wananchi wakidai wamefanyiwa vitendo vilivyo kinyume na sheria na haki za binadamu na baadhi ya askari.

Akitoa taarifa hiyo leo Desemba 21, 2023 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema wananchi hao ni pamoja na Getrude Masanja anayelalamika kufanyiwa vitendo kinyume cha sheria huko mkoani Kilimanjaro.

Sauti ya SACP David Misime .

Aidha Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi limeziona video hizo za malalamiko hayo na limeanza kuyafanyia uchunguzi mara moja wa malalamiko hayo kwa uzito mkubwa huku akiwamba wananchi kuwa watulivu kipindi hiki ambacho Jeshi hilo linafanya uchunguzi watuhuma hizo.