

25 April 2025, 5:59 pm
Kwa upande wao washiriki wa mdahalo huo wameeleza matumaini yao katika kukuza uchumi kupitia kilimo Shindani.
Na Alfred Bulahya.
Serikali imewahakikishia watanzania kuwa mashamba ya vijana wa mradi wa jenga kesho iliyo bora BBT yanafanya vizuri na kwamba vijana 12 ndio walioondolewa kutokana na kuonesha kutokuwa tayari kuwepo kwenye mradi huu.
Katibu mkuu wa wizara ya kilimo Mhe Gerald Mweli ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akifunga mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya kilimo Roundtable Afrika KRTA .
Naye Mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa kilimo Roundtable bi. Rhoda Magoiga amesema taasisi hiyo inatekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano 2025-2029 unao jikita kwenye ujenzi wa sekta ya kilimo iliyo shindaniwa.