Dodoma FM

Ihumwa watakiwa kuripoti matukio ya uhalifu

7 May 2026, 16:32

Wananchi wa eneo hilo wamekuwa hawaripoti matukio ya wizi licha ya matukio hayo kutokea mara kwa mara.Picha na mtandao.

Aidha amesema watu wa eneo hilo wamekuwa na tabia ya kuto kufuatilia kesi za wizi kutokana na kudai watu wanaofanya matukio hayo ni watu wao wa karibu.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa mtaa wa Ihumwa A wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa kituo Cha polisi katika eneo hilo na kwenda kuripoti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi wa vitu vya nyumbani.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa mtaa huo  Bw.Lameck Mbinda alipo kuwa akiongea na taswira ya habari ambapo amesema wananchi wa eneo hilo wamekuwa hawaripoti matukio ya wizi licha ya matukio hayo kutokea mara kwa mara.

Sauti ya Bw.Lameck Mbinda .

Aidha amesema watu wa eneo hilo wamekuwa na tabia ya kuto kufuatilia kesi za wizi kutokana na kudai watu wanaofanya matukio hayo ni watu wao wa karibu.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo anasema mnamo mei 3 lilitokea tukio la wizi katika mtaa huo ambapo mkazi mmoja aliibiwa vitu vyake vyote vya ndani na inadaiwa aliefanya tukio hilo ni rafiki yake wa karibu na kesi hiyo ilipo pelekwa kituoni hapo mlalamikaji hakutokea tena kuendelea na kesi hiyo.