Dodoma FM
15 June 2026, 16:41

Ni historia inayostahili kuhifadhiwa na kusimuliwa ili vizazi vya sasa na vijavyo viweze kufahamu chimbuko na urithi wa mahali wanapoishi.
Na Yussuph Hassan.
Historia ya Vilindoni inaonesha kuwa eneo hili limekuwepo kwa muda mrefu kama makazi ya watu waliotegemea kilimo na ufugaji kwa maisha yao ya kila siku.
Miongoni mwa alama muhimu za historia yake ni Shule ya Msingi Vilindoni, moja ya taasisi kongwe katika eneo hilo, iliyoanzishwa mwaka 1975.
Simulizi za vilindo vya kuhifadhia nafaka, pamoja na uwepo wa taasisi za muda mrefu kama Shule ya Msingi Vilindoni, ni ushahidi wa safari ndefu ya maendeleo ya eneo hili kutoka jamii za wakulima wa zamani hadi kuwa sehemu ya Dodoma ya kisasa.