Dodoma FM

Je kuna umuhimu wa mume na mke kuwa na elimu sawa?

27 November 2026, 17:00

Picha ni wanando wakiwa katika nyumba ya ibada na zoezi ya kuvalishana pete likiendelea. Picha na Mwananchi.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa kiwango cha elimu kati ya mme na mke si sababu ya kuzuia watu kuingia kwenye ndoa, wakisisitiza kuwa jambo la msingi zaidi ni upendo, maelewano na kuheshimiana ndani ya familia.

Na Daniel Njau.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kuwa mtu hawezi kukataa kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya tofauti ya elimu, kwani maisha ya ndoa yanahitaji ushirikiano na kuelewana zaidi kuliko kiwango cha elimu alichonacho mmoja wao.

Baadhi yao wamebainisha kuwa ingawa kuwa na elimu inayofanana kunaweza kusaidia katika mawasiliano na kufanya maamuzi ya pamoja, bado si kigezo kikuu cha mafanikio ya ndoa. Wamesema kuna ndoa nyingi zimeendelea kuwa imara licha ya wanandoa kuwa na viwango tofauti vya elimu.

Aidha, wengine wameeleza kuwa msingi mkubwa wa ndoa ni kuheshimiana, kuvumiliana na kusaidiana katika changamoto mbalimbali za maisha, wakiamini kuwa ndoa yenye heshima na maelewano inaweza kudumu bila kujali tofauti za elimu.

Ripoti ya Daniel Njau.