Dodoma FM

Uwepo wa chakula shuleni kupunguza utoro na kuongeza ufaulu               

3 September 2026, 16:34

Uwepo wa chakula shuleni kuwasaidia kusoma vizuri na kupinguza utoro wa wanafunzi mashuleni. Picha na mtandao.

Baadhi ya wazazi wamesema tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa chakula shuleni kumekuwa na mabadiliko ya taaluma kwa watoto wao kupelekea hamasa kwa wazazi ambao walikuwa hawana mwamko wa kuchangia chakula shuleni.  

Na Victor Chigwada.

Juhudi za wazazi wa kijiji cha  makang’wa  za kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni umeleta matokeo chanya kwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Akiongea na taswira ya habari mwenyekiti wa kijiji cha  makang’wa bw.aidani  mamba amesema mchakato huo wa chakula umepelekea kupunguza utoro shuleni na kupelekea wanafunzi wa shule hiyo kuwa na ari ya kusoma.

Sauti na Victor Chigwada.