Dodoma FM

Zaidi ya hekari 6000 zatengwa kwaajili ya blockfarm Kongwa

28 April 2023, 3:11 pm

Mkuu wa wialaya amewaomba madiwani kuwahimiza wananchi kuhusu suala la uhifadhi wa chakula hususani katika kipindi hiki Cha mavuno Kwani wengi wao wamekuwa wakiuza mazao Kwa kasi badala ya kuhifadhi kwaajili ya msimu ujao.

Insert 2 sec 00:34

NA Bernadetha Mwakilabi, Kongwa

Zaidi ya hekari 6000 zimetengwa kwaajili ya kilimo Cha Blockfarm ili kusaidia wananchi waweze kunufaika na kilimo Cha umwagiliaji na kuongeza upatikanaji wa chakula wilayani Kongwa.

Akiongea katika kikao Cha madiwani Cha kuwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 mkuu wa wilaya ya Kongwa mh Remidius Mwema amempongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Kwa kuweza kufanikiwa kupata eneo kubwa litakaloleta tija Kwa wananchi katika sekta ya kilimo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kongwa
Waheshimiwa madiwani na wataalam wa idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya Kongwa wakiwa katika kikao Cha madiwani Cha kuwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 . Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Akitilia mkazo suala la kilimo Cha umwagiliaji mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kongwa Mheshimiwa White Zuberi amesema kuwa licha ya eneo hilo la hekari 6000 lakini pia Kuna maeneo ya mbuga na mabwawa vijijini ambayo yanaweza kutumika katika kilimo Cha umwagiliaji.

Sauti ya diwani wa Kata ya Kongwa .

Akisoma taarifa ya mwenyekiti wa halmashauri, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya kongwa Dr Omary Nkullo amesema katika kipindi Cha robo ya tatu zaidi ya milioni 39 sawa na asilimia 10 za mapato ya ndani zilitengwa kwaajili ya mikopo Kwa wanawake vijana na wenye ulemavu, mikopo hiyo ambayo kwa sasa Serikali imesitisha mpaka itakapotangazwa tena.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya kongwa

Nae Afisa maendeleo ya jamii wilaya Kongwa Bi Pascalina Duwe ametumia wasaa huo kuomba waheshimiwa madiwani kusaidia kuwasisitiza wananchi kurejesha fedha zote walizokopa ambazo zipo nje ya muda wa marejesho.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii wilaya Kongwa.