Dodoma FM

STAMICO kuanza kuzalisha nishati mbadala

10 July 2023, 5:32 pm

Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika hilo Bwana Venance Mwase akizungumza na vyombo vya habari .Picha na Fred Cheti.

Matumizi ya mkaa na kuni yanatajwa kuchangia uchafuzi na uharibifu wa mazingira.

Na Fred Cheti.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatarajia kuanza kuzalisha  nishati ya mkaa mbadala kwa ajili ya kupikia ambao unaelezwa kuwa rafiki kwa mazingira.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika hilo Bwana Venance Mwase ambapo amesema mkaa ni rafiki kwa mazingira  na unazalishwa kwa ubora wa hali ya juu bila ya kuwa na athari za kiafya kwa mtumiaji.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo.
Mkaa huo mbadala ambao umetengenezwa na shirika la madini la Taifa. Picha na Fred Cheti.

Mkugenzi huyo ametoa  rai kwa watanzania kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanatajwa kama uchafuzi wa mazingira na kuanza kutumia nishati mbalimbali mbadala zinazozalishwa.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo.