Dodoma FM

Watanzania wahimizwa kutumia lugha ya kiswahili

2 April 2021, 9:46 am

Na; Yussuph Hans.

Imeelezwa kuwa kiswahili ni moja ya lugha iliyo enea katika Mataifa ya Afrika kutokana na jitihada mbalimbali zilizo fanyika katika kukuza lugha hiyo.

Hayo yamesema na Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA Bi. Consolata Mushi alipo kuwa akizungumza na Taswira ya habari ambapo amesema kuwa lazima kuwe na utamaduni wa Watanzania kuipenda lugha ya kiswahili kwa kuzungumza

Amesema kuwa baadhi ya watanzania wanaoishi na kusoma sehemu mbalimbali  za Afrika huona aibu kuzungumza lugha ya kiswahili na kutumia lugha nyingine suala ambalo halitoi matokeo chanya katika kukuza lugha ya kiswahili.

Aidha Bi Consolata ameishauri jamii kutokuona aibu kuzungumza lugha ya kiswahili popote Afrika, kutokana na kukua kwa lugha hiyo pamoja na jitihada za serikali zilizofanyika katika kuikuza.

Taswira ya habari imezungumza na Dkt. Stella Faustin Mwalimu wa Lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), pamoja na baadhi ya Wanafunzi kufahamu fursa gani wanaziona baada ya kuhitimu Masomo yao ambapo wamesema kuwa licha ya lugha hiyo kuwa fursa kubwa ya kuunganisha jamii za Mataifa mbalimbali , pia kumekuwa na uhitaji  wa wataalamu  wa kufundusha lugha ya Kiswahili pamoja na wakalimani  kutafsiri lugha hiyo.

Sanjari na hayo zitakumbukwa jitihada za hayati Rais Magufuli katika katika hotuba zake za kimataifa kutumia lugha ya kiswahili na hivi karibuni Rais wa Afrika Kusini Rais Cyril Ramaphosa amesema wataendelea kuenzi lugha ya kiswahili nchini kwao.