Dodoma FM

Nini kifanyike kesi za ukatili kingono zisimalizwe kifamilia?

9 August 2023, 4:19 pm

Jamii inatakiwa kuvunja ukimya kwa jamii juu ya matukio ya ukatili wa kingono unaofanywa na kuhusisha ndugu au watu wa karibu wanaoaminiwa na wazazi au walezi.Picha na Mwananchi.

Unyanyasaji unaweza kutokea katika mazingira mbalimbali ya kijamii kama vile sehemu za kazi, nyumbani, shuleni au kwenye Taasisi za kidini.

Na Mariam Matundu.

Ni aina ya unyanyasaji unaohusisha matumizi ya matamshi ya ngono ya wazi au ya siri, ikiwa ni pamoja na ahadi zisizohitajika na zisizofaa za zawadi kwa kubadilishana na faida za ngono.

Unyanyasaji wa kijinsia unajumuisha vitendo mbalimbali kama vile maneno yasiyofaa kwa jinsia nyingine.