Dodoma FM

Mfumuko wa bei za bidhaa waathiri maisha ya wananchi

14 May 2026, 15:58

Wananchi wamesema kupanda kwa bidhaa kunapelea ugumu wa maisha kukithiri.Picha na mtandao.

kupanda kwa bei ya bidhaa kunatoka na bei ya usafirishaji wa bidhaa kuwa juu pamoja na kiwango kidogo cha uzalishaji wa bidhaa kutoka viwandani.

Na Firdaus Makame.

Wananchi jijini Dodoma wamelalamikia kupanda kwa bei za bidhaa hususani bei ya vyakula hali inayowaathiri kila kisu.

Taswira ya habari imezungumza na wakazi wa mtaa wa Chinangali Jijini Dodoma ambapo wamesema kupanda kwa bidhaa kunapelea ugumu wa maisha kukithiri na kuathiri baadhi ya kaya kila siku.

Aidha wananchi hao wamesema bei za bidhaa za vyakula kama mchele , mafuta ya kupikia na unga imeongezeka kwa siku za hivi karibuni hali inayopelekea wananchi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuendana na hali ilivyo kwa sasa.

Nao baadhi ya wafanayabiashara wanadai kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa kunatoka na bei ya usafirishaji wa bidhaa kuwa juu pamoja na kiwango kidogo cha uzalishaji wa bidhaa kutoka viwandani .

Sauti za wananchi.