Dodoma FM

Mvumi Misheni waishukuru serikali kukamilika kwa shule ya sekondari

18 January 2023, 2:33 pm

Na; Victor Chigwada.                                               

Diwani wa Kata ya Mvumi Misheni Bw.Kenethi Chihute ameishukuru Serikali kwa msaada wa fedha zilizo elekezwa katika miradi mbalimbali ndani ya Kata yake

Chihute amesema kuwa kutokana na fedha hizo wamefanikiwa kuboresha upande wa miundombinu ya sekondari

pamoja na maboresho hayo ya elimu katika sekondari  amesema kuwa bado kumekuwa na changamoto kubwa upande wa shule za msingi

Ambazo zinakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo pamoja na uhaba wa madawati kwa wanafunzi

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa Kata hiyo wameishuku Serikali ya awamu ya sita kwa jitihada za kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa

Vilio vya kukosekana kwa vyumba vya madarasa ,matundu ya vyoo pamoja na uhaba wa madawati unatokana na ongezeko kubwa la wanafunzi mashuleni

Hatahivyo juhudi za makusudi zimeendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha za kuboresha miundombinu ya mashuleni