Dodoma FM

Watumishi wa ofisi ya Takwimu watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu

4 May 2023, 2:05 pm

Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande akizungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Takwimu.Picha na Alfred Bulahya.

Aidha wamejadili namna ya kuendelea kuboresha takwimu,  changamoto, Mafanikio na kutafuta ufumbuzi.

Na Alfred Bulahya.

Wafanyakazi wa ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) wameaswa kuendelea kuwa waadilifu katika uzalishaji wa takwimu ili kuliletea maendeleo Taifa.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande wakati wa  mkutano wa wafanyakazi hao uliofanyika mapema leo jijini Dodoma kwa lengo la kujadili namna ya kuendelea kuboresha takwimu,  changmoto, Mafanikio na kutafuta ufumbuzi.

Sauti ya Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande.
Watumishi wa ofisi ya Takwimu wakiwa katika mkutano huo.Picha na Alfred Bulahya.

Kwa upande wake mtakwimu mkuu wa serikali Dkt. Albina Chuwa amebainisha mafanikio na Changamoto mbalimbali katika ofisi hiyo.

Sauti ya Dkt. Albina Chuwa.

Naye kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anne Makinda amepongeza ushirikiano wa ofisi ya taifa ya takwimu huku akisema kuwa takwimu hizo zimeleta tija katika maendeleo ya nchi.

Sauti ya kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anne Makinda .