Dodoma FM

Ubovu wa barabara Mazae wakwamisha maendeleo

11 January 2021, 2:02 pm

Na,Benard Filbert

Dodoma.

Ubovu wa miundombinu ya barabara katika Kata ya Mazae Wilayani Mpwapwa imetajwa kuwa kero hali ambayo inasababisha kushindwa kufanyika kwa shughuli za kimaendeleo.
Mmoja wa mkazi wa mtaa wa mazae akizungumza na taswira ya habari amesema hivi sasa ni ngumu kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwani barabara hazipitiki kirahisi.

Ameongeza kuwa endapo zitafanyiwa marekebisho zitasaidia wakazi wa kata ya mazae kufanya shughuli za kimaendeleo kwa urahisi.
Taswira ya habari imezungumza na diwani wa Kata ya Mazae Bw.William Madanya amesema ni kweli miundombinu ya barabara katika Kata hiyo hairidhishi hivyo ipo katika mkakati wa kufanyiwa marekebisho na wakala wa barabara za Vijijini TARURA.