Dodoma FM

Wananchi Ihumwa walalamikia ubovu wa barabara

20 January 2021, 1:57 pm

Na,Victor Chigwada,

Dodoma.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ihumwa jijini Dodoma wamelalamikia ubovu wa miundombi ya barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo zimesababisha kukatika kwa mawasiliano kutokana na magari kushindwa kufika kwenye kituo cha maegesho.
Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema hali hii inawaathiri kutokana na kushukia njiani na kulazimika kuvuka kwa miguu na kutembea umbali mrefu mahali palipojaa maji.
Diwani wa Kata ya Ihumwa Bw.Edwadi Magawa ameiomba Serikali kuishughulikia changamoto hiyo ya muda mrefu kwa kuwa tayari Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alishatoa maelekezo kujengwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mratibu wa wakala wa barabara za mjini na Vijijini TARURA Mkoa wa Dodoma Bw.Lusako Kilembe amesema kuwa kwasasa wapo katika hatua za mwisho kuhakikisha barabara zote zinapitika kirahisi ndani ya Jiji katika majira yote ya mwaka.