Dodoma FM

Vijana Kongwa wapokea bonanza la afya

16 June 2023, 1:54 pm

Muuguzi Maryciana Bwana wa kituo Cha afya Ugogoni wilayani Kongwa akichukua kipimo cha Presha kwa wanafunzi Rika balehe kwenye bonanza la Afya liliilofanyika wilayani humo. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Afisa lishe wilaya Kongwa Bi. Maria Haule amesema vijana lika balehe wakike wanatakiwa kujenga utaratibu wa kula vyakula vinavyoongeza damu ili kusaidia kurudisha damu inayopotea wakati wa hedhi.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Wilaya ya Kongwa imepongeza na kushukuru wizara ya afya kwa kushirikiana na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kwa kuandaa na kuleta bonanza la afya kwa kutoa elimu na huduma za afya kwa vijana balehe wilayani humo.

Akiongea katika uwanja wa sabasaba mratibu elimu ya afya mashuleni wilaya ya Kongwa muuguzi Remija Ng’ingo amesema kuwa vijana wamevutiwa na elimu iliyotolewa kwani wamepata idadi kubwa ya mabinti waliopata chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi.

Sauti ya muuguzi Remija Ng’ingo.

Nao wanafunzi kutoka shule za sekondari zilizopo katika Kata za Sejeli Ugogoni Sagara na Kongwa wamesema kuwa wamefurahishwa na elimu ya afya ya akili na ukatili wa kijinsia kwani wao wapo kwenye hatari kubwa ya kuathiriwa na masuala hayo.

Kwa upande wake Bi faraja Mgeni kutoka wizara ya afya idara ya afya ya uzazi mama na mtoto amesema kuwa bonanza limefanyika katika mikoa ya Tanga , Morogoro, Geita, singida na Dodoma na lengo likiwa ni kutoa elimu na huduma za afya kwa vijana wenye umri wa miaka 14 Hadi 24 zikiwemo elimu za kujikinga na magojwa yasiyoambukiza na mimba za utotoni.

Sauti ya Bi faraja Mgeni .
Baadhi ya wanafunzi wa kike shule za sekondari wilayani Kongwa waliopatiwa chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Nae Bi Maureen Kunambi katibu wa afya mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi kutoka wizara ya afya ameshauri Serikali kupanua wigo kufikia mikoa mingi zaidi na kuwasaidia vijana kupata vifaa vya michezo ili kuboresha zaidi bonanza kwa awamu zijazo.

Sauti ya Bi Maureen Kunambi .