Dodoma FM

Ukosefu wa elimu ya udereva kwa bodaboda yachangia kuto kujua sheria za barabarani

20 October 2022, 12:11 pm

Na; Mariam Matundu.

Kutokupata mafunzo ya udereva katika chuoni kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda walio wengi ni sababu inayotajwa kuchangia wengi wao kutokuwa na matumizi sahihi na salama ya barabara .

Baadhi ya madereva wa pikipiki hapa Dodoma wamesema ni muhimu elimu ya sheria za barabarani ikatolewa kila wakati kwa madereva wa pikipiki kwani wengi wahana umakini wawapo barabarani .

kwa upande wake Michael Yolamu ni dereva wa pikipiki wa muda mrefu amesema kuwa mara kadhaa katika kijiwe chake cha pikipiki huwa anachukua jukumu kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara.

.

Sajenti Maritine Mangu kutoka ofisi ya mkuu wa polisi usalama barabarani kitengo cha elimu kwa umma akizungumza katika kipindi cha the morning power amesema kuwa richa ya uwepo wa sheria lakini wamejikita zaidi kutoa elimu ili kujenga uelewa kwa madereva wa pikipiki.

.