Dodoma FM

Uhaba wa maji katika kata ya Msanga wapelekea wananchi kununua maji kwa bei kubwa

16 September 2021, 12:45 pm

Na ;Victor Chigwada.

Changamoto ya uhaba wa maji katika Kata ya Msanga Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umeendelea kuwa kilio kikubwa kwa wananchi na kusababisha maji kununuliwa kwa bei kubwa.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Msanga wameiomba Serikali kuwasaidia kupata kisima cha maji safi kwani wamekuwa wakifanyiwa utafiti wa kuchimbiwa kisima cha maji bila mafanikio

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Hatibu Ramadhan amekili kuwa baadhi ya vitongoji vinapata maji kutoka Chamwino huku baadhi ya maeneo yakiwa hayana huduma hiyo

Diwani wa Kata hiyo Bw. Emmanuel Ng’ata amekiri kukosekana kwa huduma ya maji katika Kata hiyo hatua ambayo inawalazimu wananchi wa Kata hiyo kufuata huduma ya maji katika visima vilivyopo Wilayani Chamwino