Dodoma FM

BMH kuanzisha upasuaji wa moyo kwa watu wazima

11 October 2023, 9:04 am

Picha ni wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa wakishirikiana kumpongeza Dkt Stella. Picha na Mariam Kasawa.

Katika kuadhimisha Miaka 8 ya Mafanikio Hospitali ya Benjamin Mkapa zaidi ya wananchi 100 wamepatiwa huduma ya Nyonga na kupunguza gharama na usumbufu.

Na Mindi Joseph.

Katika kuadhimisha miaka 8 Hospitali ya Benjamin Mkapa inatarajia kuanzisha huduma za upasuaji wa Moyo kwa watu wazima kuanzia octoba 16 .

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema kambi hiyo wataifanya kwa kushirikiana na wadau.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika
Picha ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo. Picha na Mariam Kasawa.

Katika hatua nyingine amempongeza Dkt. Stella Malangahe ambae ni Daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ushindi wa Tuzo ya Daktari Bora wa Mwaka Nchini.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika

Kwa upande wake Dkt. Stella Malangahe ameshukuru viongozi kwa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa jitihada.

Sauti ya Dkt. Stella Malangahe.