Wananchi Dodoma watakiwa kutumia fursa zinazopatikana kujiingizia kipato
29 July 2026, 15:39

Vile vile kupitia uongozi wa jiji wanatoa mikopo na elimu bure kwa watu wote wanaotaka kujikita katika ufugaji wa samaki wa mabwawa ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa wananchi.
Na Jerome John.
Wakazi wa jiji la Dodoma wametakiwa kuzitumia fursa zinazopatikana katika maeneo yao ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao.
Afisa Mifugo na Uvuvi Jiji la Dodoma Gration Mwesiga amebainisha kuwa ufugaji wa samaki kupitia mabwawa ni fursa ya kipeke ambayo wakazi wa jiji hilo wanatakiwa kuitumia ipasavyo katika kukuza uchumi wao.
Aidha amesema kuwa kulingana na uhitaji wa kitoweo hicho upatikanaji wake umekuwa hadimu na hivyo kufanya soko la samaki kuwa muhimu sana kwa wenyeji na wageni.
Mwesiga ameeleza kuwa ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa utumia muda wa miezi sita hadi uvunaji wake na kupelekwa sokoni pia utumia gharama ndogo kulingana na eneo linalotumika katika uchimbwaji wa bwawa hilo.