Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuthibitisha taarifa kabla ya kusambaza katika mitandao

4 September 2026, 17:08

Taarifa isiyothibitishwa inaweza kuleta hofu kwa wananchi, mtu anaamini taarifa isiyo ya kweli, hivyo tunapaswa kuhakiki kabla ya kusambaza machapisho. Picha na mtandao.

Hamza Yussuph ni mtaalamu wa usalama mtandaoni (cyber security)amesema  athari za kutumwa kwa taarifa ambazo hazijathibitishwa kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kupelekea madhara makubwa kwa mtu atakae tena au kutendewa kosa hilo.

Na Ramadhan Juma.

Matumizi ya mitandao ya kijamii yameendelea kuwa sehemu muhimu ya upatikanaji na usambazaji wa taarifa kwa jamii, huku baadhi ya watumiaji wakisambaza taarifa kabla ya kujiridhisha kuhusu ukweli wake.

Hali hiyo imeibua mjadala kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza pale taarifa zisizothibitishwa zinaposambazwa na kufikia watu wengi kwa muda mfupi.

Taarifa isiyothibitishwa inaweza kuleta hofu kwa wananchi, mtu anaamini taarifa isiyo ya kweli na kufanya maamuzi na kupelekea  migogoro na chuki miongoni mwa watu.

Mmoja wa watengeneza maudhui jijini Dodoma anasema kusambambaza taarifa zisizo thibitishwa kunaweza kumuharibia mtu au taasisi sifa pia anaweza ikapelekea kufunguliwa mashtaka.

Sauti na Ramadhan Juma.