Dodoma FM

Wakazi Mwanakianga Kati walalamikia vifusi vilivyorundikana barabarani

10 July 2026, 18:04

Vifusi hivyo vimekuwa kero kubwa na chanzo cha ajali pamoja na usumbufu kwa wapita njia.Picha na Dodoma fm.

Ameomba Serikali na wadau husika wachukulie hatua za haraka ili kuondoa usumbufu unaowakabili wananchi.

Na Stephen Noel.
Wananchi wa Kijiji cha Mwanakianga Wilayani ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma wameilalamikia Serikali kushindwa kusambaza vifusi vilivyolundikwa kando ya barabara kwa zaidi ya miezi mitatu.

Akizungumza na DODOMA FM, baadhi ya wakazi wamesema vifusi hivyo vimekuwa kero kubwa na chanzo cha ajali pamoja na usumbufu kwa wapita njia kwa miguu na madereva wa magari.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanakianga Kati amekili kuwepo kwa changamoto hiyo na amesema suala hilo tayari amelifilisha katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Ofisi ya Kata kwa ajili ya utekelezaji.

Sauti ya Noel Kina.