Dodoma FM
Dodoma FM
11 May 2026, 16:22

Kituo hicho kukabiliwa na uchakavu wa majengo yake sanjali na nyumba za watumishi wa afya.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Handali wilayani Chamwino wameiomba serikali kupitia wizara ya afya kukarabati kituo cha afya kijijini hapo kwani majengo yake ni chakavu sana hali inayo hatarisha usalama wa wagonjwa.
Wakiongea na taswira ya habari wananchi hao wamesema licha ya kituo hicho kuwa na majengo chakavu pia kuna ukosefu wa jengo la mama na mtoto hali inayo walazimu wajawazito kuchanagamana na wagonjwa wengine .
Diwani wa Kata ya Handali Bw.Emmanuel Madali amekiri kituo hicho kukabiliwa na uchakavu wa majengo yake sanjali na nyumba za watumishi wa afya
Aidha Madali amesema tayari taarifa za uchakavu wa majengo ya kituo hicho wameziwasilisha katika Halmashauri ya wilaya na ngazi ya mkoa kuomba ukarabati wa majengo hayo ya kituo Cha afya.