Wachimbaji Nayu walalamika kukosa vifaa kinga
25 June 2026, 17:26

Kemikali migodini hutumika katika kuchuja, kutenganisha, na kuyeyusha madini kama dhahabu na shabakutoka kwenye miamba, pamoja na kutibu maji machafuKemikali kuu inayotumika ni Zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika migodi ya Norni Dabalo na Nayu Mpalanga wameeleza kukosekana Kwa vifaa Kinga na kupelekea baadhi yao kuathirika na kemikali ya zebaki.
Imeelezwa kemikali hiyo inayotumiwa zaidi na wachimbaji wadogo imekuwa chanzo cha kubabuka ngozi zao na vidonda katika mikono Yao.
Hata hivyo wameendelea kusisitizana kuwa ni vyema Kila mtu kujali afya yake Kwa kuchukua tahadhari kabla ya hatari
Renatusi kumila mtaalamu na mkemia wa migodini amekiri matumizi ya kemikali migodini yasipo tumika bila Kinga ya naweza kuleta madhara ya afya Kwa wachimbaji
Kumila amesema kuwa kupitia vumbi la kamekali kuganda kwenye ngozi ambayo ikitoa jasho itapelekea ngozi kuathirika ama vumbi pia huathiri mapafu na wakati mwingine kemikali zikiingia Kwa njia ya kinywa zinaweza kuleta madhara ya kupoteza maisha