Dodoma FM

Waziri Mkuu atoa Tamko mradi uboreshaji milki za Ardhi

28 November 2023, 6:00 pm

Picha ni viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo. Picha na Seleman Kodima.

Mradi huu unatekelezwa  katika kipindi cha miaka mitano (5) na una vipengele vinne (4) ambavyo ni Kuongeza  Usalama wa Milki; Kuimarisha Mifumo ya Taarifa za Ardhi; Kujenga Miundombinu ya  Ardhi na Usimamizi wa Mradi.

Na Seleman Kodima.

Wakurugenzi wa Halmashaurii nchini wametakiwa kuhakikisha katika kipindi hiki cha maandalizi ya Bajeti ya  mwaka 2024/25 wanatenga fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi ili kuendeleza utekelezaji  wa mradi  wa kuboresha usalama wa Miliki za Ardhi katika maeneo  ambayo mradi huo  haujafika.

Pia katika maeneo ambayo Mradi huo unatekelezwa Wakurugenzi wa Halmashauri wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Timu za  Utekelezaji wa Mradi wa LTIP .

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. kassim majaliwa ambapo Waziri wa Ardhi Jerry Silaa alimwakilisha katika Mkutano wa kitaifa   mkuu wa   wadau wenye lengo la kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa Miliki za Ardhi _LITP uliofanyika katika  ukumbi wa Mabele – Mabeyo Complex Jijini Dodoma .

Sauti ya Waziri wa Ardhi Jerry Silaa.
Picha ni Waziri wa Ardhi Jerry Silaa alimwakilisha katika Mkutano wa kitaifa   mkuu wa   wadau wenye lengo la kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa Miliki za Ardhi _LITP. Picha na Seleman Kodima.

Nae Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Waziri wa Ardhi Jerry Silaa   akitoa taarifa ya Mradi huo amesema moja ya changamoto inayoukabili mradi huo katika  utekelezaji kwa sasa ni wanufaika wengi ambao maeneo yao tayari  yameshafanyiwa urasimishaji kushindwa kupata hati zao kwa  kukosa namba za NIDA ambazo ndizo zinazotambulika katika mfumo  wa  umilikishaji.

Sauti ya mh.Waziri wa Ardhi Jerry Silaa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amepongeza mradi huo ambao unaenda  kutatua changamoto zinazohusiana na masuala ya ardhi  hasa kwa Mkoa wa Dodoma.

Suti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule .

Januari 21  2022 Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba  na Maendeleo ya Makazi ilisaini makubaliano na Benki ya Dunia ya mkopo wa Shilingi  bilioni 346 sawa na dola za kimarekani milioni 150 kwa ajili ya utekelezaji wa  Mradi wa Kuboresha Usalama wa Miliki za Ardhi nchini.