Dodoma FM

Wanawake watakiwa kutetea haki za watoto

9 March 2023, 5:29 pm

Wanawake wakiwa katika mkutano wa siku ya wanawake wilayani Kondoa hapo jana. Picha na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Mkoa amewataka wanawake kusimama imara katika jamii kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutetea haki za watu wenye ulemavu.

Na Mariam Kasawa.

Wanawake wametakiwa kusimama imara kutetea haki za watoto pamoja na haki za watu wenye ulemavu Nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya wanawake yaliyo fanyika jana Kimkoa wilayani Kondoa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule amewataka wanawake pamoja na mabinti wote walio shindwa kumliza masomo yao wajitokeze kusoma.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule

Nae kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, Suzana Kaganda akizungumza katika maadhimisho hayo amewakumbusha wananchi kutumia vituo vya polisi katika kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Sauti ya kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, Suzana Kaganda

Akitoa salamu zake Katika maadhimisho hayo mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt.Ashatu Kijaji alikuwa na haya yakusema.

Sauti ya mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji